• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miji ya pwani yatakabiliwa na tishio kubwa zaidi la mafuriko ifikapo mwaka 2050

    (GMT+08:00) 2017-06-08 19:23:42

    Wanasayansi wa Marekani wamesema kuongezeka kwa joto duniani kutasababisha kuinua kwa usawa wa bahari, na ifikapo mwaka 2050, uwezekano wa kutokea kwa mafuriko makubwa ambayo sasa kwa wastani yanatokea kila baada ya miaka 50 utaongezeka kwa mara moja.

    Kikundi cha utafiti cha tawi la Chicago la Chuo Kikuu cha Illinois cha Marekani kimetoa makadirio hayo kwenye gazeti la Scientific Reports la Uingereza baada ya kuchambua athari ya mambo mbalimbali yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, mawimbi, dhoruba na shinikizo dogo la hewa.

    Wanasayansi wengi wanaona kuwa kuongezeka kwa joto duniani kutasababisha barafu kuyeyuka, na usawa wa bahari duniani utainuka kwa sentimita 10 hadi 20 katika makumi ya miaka ijayo.

    Kiongozi wa kikundi cha utafiti Prof. Sean Vitousek alisema usawa wa bahari ukiinuka kwa sentimita 5, miji ya Mumbai na Gorge nchini India na Abidjan nchini Cote d'Ivoire itakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya mafuriko, na ukiinuka kwa sentimita 10, miji ya Shanghai, London na New York pia itaathiriwa na mafuriko.

    Prof. Vitousek alisema hatua za kukabiliana na mafuriko ni pamoja na kuhamisha miji ya pwani na kutenga fedha nyingi katika ujenzi wa miradi ya kukinga mafuriko pwani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako