• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Craig Shakespeare awa Kocha mpya wa Leicester City

    (GMT+08:00) 2017-06-09 09:09:43

    Leicester City wamemteua kaimu meneja Craig Shakespeare kuwa meneja kamili wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.

    Alikuwa amepewa kazi ya kuwa meneja wa muda Februari baada ya kufutwa kazi kwa Claudio Ranieri. Shakespeare, mwenye miaka 53, ambaye amefanya kazi kama kaimu au mkufunzi msaidizi pekee, alikuwa msaidizi wa Ranieri baada ya kujiunga na klabu hiyo chini ya meneja wa awali Nigel Pearson.

    Shakespeare alishinda nane kati ya mechi 16 alizokuwa kwenye usukani Leicester msimu uliopita, na kuongoza pia klabu hiyo kufika robo fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

    Kama mabingwa watetezi Ligi ya Premia, Leicester walikuwa alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja wakiwa na mechi 13 zilizosalia Ranieri alipoondoka.

    Lakini Shakespeare aliwasaidia kushinda alama 23, miongoni mwa hizo akizizoa kwa kushinda mechi zake tano za kwanza na kuwawezesha kumaliza wakiwa nafasi ya 14.

    Leicester waliondolewa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Atletico Madrid.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako