• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mzozo wa kidiplomaisa kati ya Qatar na nchi za kiarabu waendelea kukua

    (GMT+08:00) 2017-06-09 09:46:20

    Mwenyekiti wa Baraza la haki za binadamu la Qatar Bw Ali bin Sumaikh Al Marri amesema hatua za kukata mawasiliano ya anga, barabara na baharini zilizochukuliwa na nchi za kiarabu baada ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Qatar, zimekiuka sheria za kimataifa na haki za binadamu, pia zimeathiri vibaya utaratibu wa kijamii, mawasiliano ya kibiashara na kiutamaduni kwenye kanda hiyo.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw António Guterres jana alitoa taarifa kuzitaka nchi husika kuondoa tofauti kwa njia ya kidiplomasia, ili hali isije kuwa mbaya zaidi.

    Kwa mujibu wa amri ya wizara ya ulinzi ya Qatar, vikosi vya jeshi la anga la Qatar vinavyoshiriki kwenye operesheni ya kijeshi nchini Yemen vilirudi jana nchini Qatar.

    Wizara ya mambo ya nje ya Senegal juzi imetoa taarifa ya kumrudisha balozi wake nchini Qatar, ili kuunga mkono msimamo wa Saudi Arabia na nchi husika za kiarabu kukata uhusiano wa kibalozi na Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako