• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kama hatua hazitachukuliwa, takataka za plastiki zitakuwa nzito zaidi kuliko samaki wote baharini

    (GMT+08:00) 2017-06-09 18:12:58

    Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Bw Erik Solheim ametoa wito kuzitaka nchi nyingi zaidi kupunguza takataka za plastiki ili kuifanya bahari iwe safi zaidi.

    Mkutano wa kwanza wa bahari wa Umoja wa Mataifa unafanyika kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 9 katika makao makuu ya umoja huo, na uchafuzi wa bahari ni suala linalofuatiliwa kwenye mkutano huo.

    Bw. Solheim amepokea ombi lililosainiwa na mamilioni ya watu duniani ambalo linazitaka nchi mbalimbali ziache matumizi ya vitu vya plastiki vinavyotumiwa kwa mara moja tu katika miaka mitano ijayo. Bw. Solheim alisema hivi sasa nchi zaidi ya 20 zimeahidi kupunguza takataka za plastiki, lakini wanahitaji nchi nyingi zaidi kutoa ahadi hiyo ili kupunguza takataka zinazoingia baharini kwa kiasi kikubwa.

    Takwimu zinaonesha zaidi ya tani milioni 8 za takataka za plastiki zinazoingia baharini kila mwaka, zimeathiri vibaya viumbe wa baharini, uvuvi na utalii, na kusababisha hasara ya dola za kimarekani bilioni 8. Inakadiriwa kuwa takataka za plastiki zinasababisha vifo vya mamilioni ya ndege wa baharini, laki moja ya mamalia wa habarini na samaki wengi sana wasioweza kukadiriwa. Utafiti unaonesha kuwa kama binadamu hawatachukua hatua kupunguza takataka, ifikapo mwaka 2050, takataka za plastiki zitakuwa nzito zaidi kuliko samaki wote baharini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako