• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapunguza ada ya leseni ya magari

    (GMT+08:00) 2017-06-09 19:16:48
    Serikali ya Tanzania imetangaza kufuta ada ya leseni ya magari, kupandisha bei ya vinywaji baridi na bia, mafuta na kupunguza ushuru wa mazao unaotozwa na halmashauri za wilaya kutoka asilimia 5 hadi 3.

    Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema serikali inafanya marekebisho ya viwango maalumu vya ushuru kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa kiwango cha mfumuko wa bei cha asilimia tano.

    Hata hivyo, Dk Mpango ameongeza kuwa kwa kuzingatia mkakati wa taifa kukuza uchumi wa viwanda, baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini hazitafanyiwa marekebisho hayo. Dk Mpango alieleza kuwa ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi unapandishwa kutoka Sh 58 kwa lita hadi Sh 61 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 3 kwa kila lita.

    Aidha, ushuru wa bidhaa kwenye maji ya kunywa yaliyosindikwa kwenye chupa yaliyoagizwa kutoka nje kutoka Sh 58 kwa lita hadi Sh 61 kwa lita ikiwa ni ongezeko la Sh tatu kwa lita. Amesema ushuru wa bidhaa kwenye maji yanayozalishwa nchini utabaki kuwa shilingi 58 kwa lita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako