• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NASA yachagua wanaanga wapya 12

    (GMT+08:00) 2017-06-13 11:11:52

    Shirika la anga ya juu la Marekani NASA limetangaza kuchagua wanaanga wapya 12, ambao baada ya kupewa mafunzo watafanya kazi katika kituo cha anga ya juu cha kimataifa na kufanya uchunguzi wa anga ya mbali.

    Wanaanga hao wenye umri kati ya miaka 29 hadi 42 ni pamoja na wanaume 7 na wanawake watano, baadhi yao ni madaktari, wahandisi, wasaidizi wa profesa, wanafunzi, marubani na maofisa wa jeshi.

    NASA linasema kuanzia Agosti mwaka huu wanaanga hao wapya watapewa mafunzo ya miaka miwili, yakiwemo mafunzo kuhusu mifumo ya vyombo vya safari ya anga ya juu, kutembea kwenye anga ya juu, ushirikiano na wanaanga wengine, lugha ya Kirussia na ustadi mwingine.

    Tangu mwaka 1959 hadi sasa kwa ujumla NASA imeandikisha kundi la 22 la wanaanga lenye waananga 350. Masharti ya kuwa wanaanga wa NASA ni pamoja na kuwa na uraia wa Marekani, shahada ya kwanza ya uhandisi, biolojia, fizikia au hesabati, uzoefu wa kazi wa zaidi ya miaka mitatu, uzoefu wa kuendesha ndege kwa zaidi ya saa 1000. Kuanzia Desemba mwaka 2015 hadi Februari mwaka 2016, Wamarekani elfu 18.3 walitoa ombi la kuwa waananga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako