• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hong Kong yawa mwanachama mpya wa AIIB

    (GMT+08:00) 2017-06-13 18:01:04

    Serikali ya mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong nchini China imesema kuwa mkoa huo umekuwa mwanachama mpya wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, AIIB baada ya kumaliza utaratibu wote wa kisheria unaotakiwa.

    Katibu wa fedha wa serikali ya mkoa wa Hong Kong Paul Chan amesema, kumalizika mapema kwa mchakato wa kujiunga na Benki hiyo kunaonyesha utayari wa mkoa huo wa kuunga mkono uendeshaji wa AIIB.

    Katibu huyo ataongoza ujumbe wa Hong Kong kwenye mkutano wa pili wa mwaka wa Bodi ya Wakurugenzi wa AIIB utakaofanyika kuanzia ijumaa wiki hii mkoani Jeju, Korea Kusini, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Hong Kong kushiriki kama mwanachama wa Benki hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako