• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Uganda na Tanzania kujenga reli yenye uwezo wa kuendeshwa na umeme

  (GMT+08:00) 2017-06-13 19:16:07

  Uganda na Tanzania zimeamua kujenga reli yake ya kisasa yenye uwezo wa kuendeshwa na umeme na kuanza kutumia umeme kwenye treni zake pindi tu watakuwa na kawi ya kutosha.

  Mratibu wa mradi wa SGR wa Uganda Kasingye Kyamugamba amesema wameamua kuwezesha treni yao kuendeshwa kwa umeme kwani miradi ya kawi inayoendelea kwa sasa ya Karuma na Isimba itazalisha kawi ya kutosha

  Nchini Kenya aidha waziri wa uchukuzi nchini humo James Macharia amesema baadaye watatumia umeme kuendesha treni zake mpya kwa gharama ya dola milioni $480 ili kuweka miundo mbinu inayohitajika.

  Tayari reli ya Kenya ya kisasa kutoka Mombasa hadi Nairobi ya kilomita 472 inahudumu na awamu ya pili ya ujenzi wa reli kuelekea Naivasha inatarajiwa kuanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako