• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaadhimisha siku ya kimataifa ya Albino

    (GMT+08:00) 2017-06-14 09:58:31

    Kenya imeungana na mataifa mengine duniani kusherehekea watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi yaani (albino).

    Katika sherehe hizi zilizofanyika Embu Kenya ,wizara ya jinsia ,utamaduni na jamii nchini Kenya imeanzisha vituo maalum va kuwapa albino ujuzi wa ujasiriamali na kufanya biashara za taaluma tofauti ili wajiimarishe kiuchumi.

    Maudhui ya sherehe ya mwaka huu yalikua na ujumbe mzito "kusonga mbele na maisha ya matumaini"

    Wito ukiwa "tunataka fursa sio kutengwa"

    Ikiwa ni siku maalum mara moja kila mwaka,jamii ya albino imeungana pamoja na kufanya maandamano katika mji wa Embu wakitoa mwito wa kutaka kukubalika na kujumuishwa katika fursa za maisha na maendeleo kama binadamu wengine.

    Suala kuu za sherehe hizi mwaka 2017 lilizingatia mikakati ya albino waishi maisha bora kiuchumi.

    Mwenyekiti wa chama cha albino nchini Kenya Isack Mwaura , amepongeza juhudi za serikali kushuhulikia changamoto za albino kama vile kuwapa fursa za ajira na masomo na kuwasaidia kwa huduma za afya.

    "tumekuja huku kuwafikia albino wa mashinani ,Serikali ya Kenya imefanya kazi nzuri kupunguza changamoto zetu,sasa kuna zaidi ya albino elfu 3 wanaopata huduma bora maisha ikiwemo kupata fursa za kazi na matibabu"

    Kwa mujibu wa utafiti wa sekta ya afya albino ,nchini Kenya wanatatizika zaidi na ukosefu wa dawa za macho na miwani za kuwakinga na jua na ukosefu wa kujumuishwa kikamilifu kiuchumi.

    Serikali kupitia wizara ya jinsia ,utamaduni watoto na masuala ya jamii, imezindua rasmi vituo maalum vya kutoa mafunzo ya ujasiriamali na biashara kwa albino nchini Kenya.

    Afisa mkuu wa idara hii katika kaunti ya Kirinyaga Jane Nyaga ,amewataka albino kujitokeza na kutumia fursa hizi zitakazobadilisha maisha yao na kuwapa ujasiri na kujiamini.

    "Mpango huu wa kipekee umepokelewa vizuri sana,albino wametaka liendlee ,hili ndio suluhisho la tatizo la maisha duni kwa albino,tunalenga kufikia albino zaidi ya elfu 10 katika mpango huu mwaka ujao kuwapa mafunzo na ujuzi"

    Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku hii ya kuwapa matumaini albino,jambo linaloendelea kuwapa hofu kuu albino ni usalama wao kutokana na watu wenye itikadi mbaya za kutaka kuwaua kwa ajili ya viungo vyao.

    Serikali ya Kenya pia imeanzisha kampeini kwa machifu wote nchini Kenya kuelimisha jamii kuchunguza na kuwatia mbaroni wahalifu hao.

    Huyu hapa ni chifu wa manispaa ya Embu Titus Mugambi.

    "jambo la kwanza ni ukijaribu kuwaua albino ni hatia, na kuvunja sheria. tuna changamoto ya kuwalinda lakini tutahakikisha tunawaelimisha jamii na kuwachukulia hatua wahalifu"

    Maelfu ya albino walijitokeza na kuungana kwa maandamano ya kusherekea siku hii.

    Nlijumuika nao ili kufahamu yaliyomo katika fikra zao.

    Mary Emaculate aliangazia ombi lao la kutaka kupewa fursa za ajira .

    'tumekua na matatizo lakini tunajitahidi ,mtu wa albino ana talanta pia anaweza kufanya kazi"

    Licha ya hatua kubwa iliyopigwa kwenye maendeleo ya albino unyanyapaa unasalia kikwazo kikuu kwao kama anavosimulia James ambae ni mhandisi

    "stigma bado inatutatiza sehemu tofauti Kenya,tungepata viongozi wawakilishi wa albino kwenye serikali kuangazia hili'

    Nae Joseph Kagunda ameangazia namna afya na matibabu ya ngozi, macho na masikio inavowahangaisha wengi

    "utakuta kwamba tuakwenda check up ya ngozi na macho kwa sababu ,bila hivyo tunaweza kufariki na saratani,tunataka serikali iendelee kusaidia kwa hili'

    Kiongozi wa kina mama albino Embu Jackline amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa usalama wao

    "hili jambo liko na liko linafanyika kwa siri , wenzetu wamefariki wamepoteza viungo vyao na wengine tumeponea kunyakuliwa, inatuweka hofu sana,hata familia zetu zinatutia hofu'

    Wakati wa sherehe hii bado Kenya haijapata idadi kamili ya albino kwani ombi lao la kutaks kujuumuishwa kwenye sensa yao maalum halijapitishwa kams anavosema Isack Mwaura.

    Yote tisa Kenya inajivunia nyadhfa kadhaa za albino uongozini kama Isack mwaura mbunge mteule,Ngugi Mumbi wakili katika mahakama kuu na wengineo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako