• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Mradi wa franc bilioni 17.2, ambayo utasaidia vijana 40,000 katika ujuzi wa utayarishaji wa kazi

  (GMT+08:00) 2017-06-14 20:07:17

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) limeanzisha mradi wa franc bilioni 17.2, ambayo utasaidia vijana 40,000 katika ujuzi wa utayarishaji wa kazi ifikapo mwaka wa 2021.

  USAID ilizindua kongamano la Huguka Dukore mjini Kigali nchini Rwanda ili kuwezesha Vijana wa Kimisagara kwa Maendeleo ya Kimataifa.

  Mpango huu ni wa kuwezesha vijana kupata ajira, kuanza biashara zao ndogo ndogo, au kufuata elimu zaidi.

  Mpango huu utatekelezwa na Kituo cha Maendeleo ya Elimu (EDC) katika muda wa miaka mitano.

  Balozi wa Marekani nchini Rwanda, Erica Barks-Ruggles, amesisitiza umuhimu wa serikali ya Marekani kushirikiana na Rwanda ili kuhakikisha kuwa vijana wake wana nafasi na ujuzi inayohitajika kuendesha maendeleo ya kiuchumi na kujenga maisha yao ya baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako