• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mratibu wa chama cha Republican kwenye bunge la Marekani yuko katika hali mbaya baada ya kupigwa risasi

    (GMT+08:00) 2017-06-15 10:35:29

    Mratibu wa chama cha Republican kwenye bunge la Marekani Bw Steve Scalise yuko katika hali mbaya baada ya kupigwa risasi jana asubuhi katika uwanja wa mpira wa besiboli, jimboni Virginia.

    Mshambuliaji anayetambuliwa kwa jina la James Hodgkinson III, mwenye umri wa miaka 66 kutoka Illinois, ameuawa kwa kupiwa risasi na polisi. Wengine watano wamejeruhiwa kwenye tukio hilo.

    Tukio lingine la ufyatuaji risasi lililotokea jana katika kituo cha UPS mjini San Francisco limesababisha vifo vya watu wanne, na wengine sita kujeruhiwa.

    Msaidizi wa mkuu wa polisi wa San Francisco Bw. Toney Chaplin amesema, mshambuliaji alijiua kwa kujipiga risasi wakati wa kukabiliana na polisi, na kwamba mshambuliaji na waliopigwa risasi wote ni wafanyakazi wa UPS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako