• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachangia mfuko wa misaada kwa wanafunzi wa Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-06-17 17:49:17

    Ubalozi wa China nchini Rwanda umetoa mchango wa fedha kwa mfuko wa Imbuto mjini Kigali ili kuuunga mkono mfuko huo kutekeleza mradi wa kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi.

    Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Bibi Sandrine Umutoni alisema wanaridhika na uhusiano wa kiwenzi kati ya mfuko huo na China ulioendelea kwa miaka kadhaa.

    Wanafunzi 100 wenye uwezo mkubwa wa kujifunza watanufaika na mchango huo.Mradi huo wa kutoa misaada ya masomo ulioanzishwa mwaka 2003 umewasaidia wanafunzi zaidi ya 7000 wa shule za sekondari kumaliza masomo yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako