• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yasajili zaidi ya wakimbizi wapya 54,000 katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2017-06-18 17:37:32

    Ethiopia imeongeza kusajili wakimbizi 54,107 kuanzia mwezi Januari hadi Mei mwaka huu, wengi wao wanatoka Eritrea, Sudan Kusini na Sudan.

    Takwimu ilitolewa na idara ya mambo ya wakimbizi na waliorejea nchini ya Ethiopia ARRA Jumamosi katika mji mkuu Addis Ababa ambapo nchi hiyo inajiandaa kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani Juni 20 katika kanda ya Gameblla ambayo ni makazi ya wakimbizi wengi toka Sudan.

    Naibu mkurugenzi wa idara hiyo Zeynu Jemal amesema kuna jumla ya wakimbizi milioni 65 duniani na Ethiopia ni moja ya nchi tano zinazoongoza kwa kuwa na wakimbizi wengi duniani.

    Ethiopia kwa sasa ni mwenyeji wa wakimbizi zaidi ya 850,000 kutoka nchi 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako