• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Walimu wa Kenya watarajiwa kuongezwa mishahara

    (GMT+08:00) 2017-06-19 10:11:03

    Ni afueni kwa walimu wa shule za umma nchini Kenya baada yao kuongezewa mishahara na tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC. Kuanzia mwezi Julai mishahara ya walimu inatarajiwa kuongezeka baada ya SRC na miungano ya kutetea haki za walimu kutia sahihi mkataba wa makubaliaano kuhusu nyongeza hiyo.

    Ndio wimbo ambao umekuwa ukitikisa mawimbi ya taifa la Kenya, siku nenda siku rudi. Walimu wakiandamana kudai haki yao, ya nyongeza ya mishahara. Na sasa, malalamishi yao hatimaye yamesikilizwa. Ijumaa iliyopita, muungano wa kitaifa wa walimu KNUT, uliingia kwenye mkataba na wizara ya Elimu wa kuwaongeza walimu mishahara kuanzia tarehe mosi mwezi Julai mwaka huu. Nyongeza hii italipwa kwa awamu mbili, kuanzia tarehe mosi mwezi ujao hadi tarehe 30 mwezi Juni mwaka wa 2021.

    Wakuu wa muungano wa KNUT wakiongozwa na Wilson Sossion walielezea furaha yao baada ya hatua hii ambayo itawafaa sana walimu.

    'Tunaamini kwamba kuanzia leo, siasi za mkataba wa malipo ya walimu zitakoma. Kwa sasa walimu wajiandae kwa mishahra mipya kuanzia kuanzia tarehe moja mwezi Julai. Mkataba huu unaenda kuwatoa walimu kwenye hali ambayo ilionekana kuwa ya utumwa na kuanza kufurahia jasho lao'

    Hata hivyo kwa walimu ambao si wananchama wa muungano wowote watahitajika kulipa faini ili kufurahia matunda haya. Mudzo Nzili ni Mwenyekiti wa Muungano wa kitaifa walimu KNUT.

    " Wale ambao si wanachama watapigwa faini kidogo ili wanufaike..'

    Kuanzia tarehe mosi Julai, kutakuwa na mpangilio mwingine mpya wa malipo ya walimu, kuanzia vitengo vya B5 hadi D5. Mwalimu wa kitengo cha B5 atalipwa shilingi 21,757 na wa juu akilipwa shilingi 27,195.

    Mwalimu wa chini wa kiwango cha C3 atalipwa shilingi 43,154 na wa wa juu akilipwa shilingi 53,943.

    Mwalimu wa chini kabisa katika kiwango cha D5 atalipwa shilingi 131,380 na wajuu akilipwa shilingi 157,656.

    Historia ya migomo ya walimu nchini Kenya ilianza mwaka wa 1962, mwaka mmoja tu kabla ya Kenya kupata Uhuru wake. Kutiwa saini kwa mkataba wa nyongeza ya mishahara kwa walimu wote wa umma ni mwamko mpya katika sekta ya elimu nchini Kenya, matunda mabayo wakuu wa KNUT wametaja kuwa safari yenye panda shuka nyingi.

    Kwa sasa, maandamano ya walimu barabarani yatazikwa kwenye kaburi la sahau baada ya matakwa yao kutekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako