• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Si ruhusa watu kubaguliwa kwa misingi ya dini na kikabila, asema Rais Uhuru Kenyatta

    (GMT+08:00) 2017-06-20 09:24:33
    Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa mashirika na shule za umma zinazowabagua wafanyikazi na wanafunzi kwa misingi ya kikabila na kidini.

    Rais Kenyatta amesema yoyote atakayepatikana na makosa hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

    Akizungumza jana wakati alipokutana na jamii ya wakorino katika uwanja wa michezo wa Nyayo jijini Nairobi,Rais Uhuru Kenyatta alisema Kenya ni taifa huru linalojali na kuheshimu dini zote kikatiba,kwa hivyo si ruhusa kwa yeyote kunyanyaswa kwa sababu ya misimamo yake ya dini au kabila.

    "Kuna vyuo vingine na waajiri ambao wanabagua watu.Katiba yetu imesema kila mtu ana uhuru wa kuabudu"

    Rais Kenyatta alisema jambo la msingi linalofaa kuzingatiwa hususan wakati huu nchi inapoelekea kufanya uchaguzi mkuu mwezi Agosti ni amani na usalama,na sio kubaguana kwa misingi ya kikabila na dini.

    Rais Kenyatta amesema katiba imeweka wazi kuhusu uhuru wa kuabudu na kwamba ubaguzi kwa misingi ya dini au kabila haukubaliwi.

    "Uhuru wa kuabudu umehakikishwa katika katiba yetu.Hatutaki kusikia mtu akisema ati kwa sababu wewe ni mkorino haufai kwenda shule fulani.Katiba imetuambia kwamba hauwezi kubagua kwa misingi ya umri,kabila au dini."

    Wakati huo huo Rais Kenyatta amesema taasisi ambazo zinabagua wanafunzi au wafanyakazi na kuwazuia kufuata maamrisho ya dini zao zitachukuliwa hatua za kisheria.

    "Kama kuna shule ambayo inapewa pesa na serikali na inazuia wakenya wengine kuingia katika shule hiyo tutakata ufadhili waserikali kwa shule hiyo halafu tutawachukulia hatua wenye makosa.Muislamu hazuiwi kuvaa hijab,kalasinga hazuiwi kuvaa kilemba,kwa nini mkorino azuiwe kuvaa kilemba"

    Aidha Rais Kenyatta ametoa onyo kali kwa viongozi wa kisiasa wanaojaribu kuwagaanya wakenya kwa misingi ya kikabila,mbinu ambayo ilitumiwa zamani kusababisha ghasia.

    "Sisi tulisema mambo mawili ambayo ni ya muhimu,na kila pahali tumekuwa tukihubiri mambo hayo.Kuna wenzetu ambao tunashindana nao,wao wnafanya mashindano ya ukabila wala sio sera.tunataka amani"

    Rais Kenyatta amewataka wakenya kuishi kwa amani,umoja na utangamano na kuepuka ghasia wakati wa uchaguzi mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako