• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yazindua mpango mpya wa kuwahusisha wakimbizi kwenye mambo ya fedha

    (GMT+08:00) 2017-06-20 09:56:24

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR kwa kushirikiana na serikali ya Rwanda, wamezindua mpango mpya wenye lengo la kuwashirikisha wakimbizi kwenye mambo ya fedha.

    Mpango huo uliozinduliwa siku moja kabla ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya wakimbizi unatarajiwa kuwawezesha wakimbizi kujitegemea kiuchumi kwa kutumia miradi ya kujipatia fedha, kupitia misaada na mikopo.

    Waziri wa Rwanda anayeshughulikia usimamizi wa majanga na wakimbizi Seraphine Mukantabana amesema fedha hizo zitatolewa kwa mfuko wa mzunguko.

    Mwakilishi wa UNHCR nchini Rwanda Bw Saber Azam amesema hatua hiyo ya Rwanda inafuatia ahadi iliyotolewa na serikali ya Rwanda kwenye mkutano wa kilele uliofanyika mjini New York, kwamba itaruhusu wakimbizi kuwa sehemu ya maendeleo ya uchumi na jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako