• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika mashariki ziko kwenye hatari ya kukumbwa na msukosuko wa kibinadamu

    (GMT+08:00) 2017-06-20 09:56:43

    Nchi za Afrika Mashariki na za pembe ya Afrika ziko kwenye hatari ya kukumbwa na msukosuko mkubwa wa kibinadamu kutokana na upungufu mkubwa wa chakula na maji.

    Shirika la hisani la Christian Aid limetahadharisha kuwa kama hakutakuwa utoaji wa chakula cha msaada, watu milioni 20 nchini Sudan Kusini, Ethiopia, Kenya na Somalia wako kwenye hatari ya kukumbwa na njaa.

    Mkuu wa ofisi ya mipango kwa Afrika wa Christian Aid Bw Maurice Onyango amesema mvua za kukatisha tamaa za hivi karibuni nchini Ethiopia na Kenya zimefuta matumaini ya kujaa kwa vyanzo vya maji, malisho kuongezeka na kuwa na mavuno ya kutosha.

    Mpaka sasa ni Sudan Kusini peke yake ndio imetangaza kukumbwa na baa la njaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako