• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yataka Djibouti na Eritrea zijizuie katika mpaka

    (GMT+08:00) 2017-06-20 10:27:04

    Katibu mtendaji wa IGAD Bw. Mahboub Maalim amezitaka Djibouti na Eritrea zijizuie katika mpaka kati yao.

    Taarifa iliyotolewa na IGAD inasema Bw. Maalim anafuatilia sana maendeleo ya tukio la kuondoka kwa kikosi cha kulinda amani cha Qatar kwenye mpaka kati ya Djibouti na Eritrea, amezitaka nchi hizo mbili zijizuie ipasavyo kwa ajili ya utatuzi wa suala hilo.

    Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bw Moussa Mahamat, amesema Umoja wa Afrika unashirikiana na serikali za pande mbili ili kuunda tume ya kuchunguza hali ya kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako