• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Taswira ya ushirikiano wa baharini kwa ujenzi wa mradi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja yatolewa

  (GMT+08:00) 2017-06-20 18:57:00

  Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China na idara ya bahari ya China zimetoa kwa pamoja waraka wa "Taswira ya ushirikiano wa baharini kwa ujenzi wa mradi wa 'Ukanda Mmoja na Njia Moja'".

  Waraka huo uliotolewa hivi karibuni unalenga kusukuma mbele utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa katika eneo la baharini, kufanya ushirikiano wa pande zote na nchi zilizo kando ya Njia ya Hariri Bahari ya Karne ya 21, kuanzisha jukwaa wazi la ushirikiano, na kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kunufaishana kwenye mambo yanayohusu bahari.

  Waraka huo umetaja kanda tatu za kiuchumi baharini, ambazo wa kwanza unaanzia hapa China, kupitia bahari ya India na Afrika na mwishowe kufikia bahari ya Mediterranean, wa pili unaunganisha China, Oceania na bahari ya Pasifiki ya Kusini, na wa tatu unaunganisha China na Ulaya kupitia bahari ya Arctic.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako