• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Wafanya biashara wa Miraa Kenya wanataka kusafirisha bidhaa zao kupitia uwanja wa ndege wa Isiolo

    (GMT+08:00) 2017-06-21 19:09:55

    Wafanya biashara wa Miraa kutoka eneo la Nyambene, kanti ya Meru nchini Kenya sasa wanataka bidhaa zao hizo zisafirishwe kwenda Somalia kupitia kwa uwanja mpya wa ndege wa Isiolo.

    Uwanja huo unatarajiwa kufunguliwa ndani ya siku chache zijazo,

    Kwa sasa wafanyabiashara hao wanasafirisha miraa kupitia uwanja wa Wilson katika mji mkuu Nairobi.

    Aidha mashirika ya kilimo katika maeneo ya Timau na Nyeri yanatarajia kuutumia uwanja huo kusafirsha bidhaa zao kama vile maua matunda na mboga kwenda Ulaya. Uwanja huo ulijengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7 na unatarajiwa kusaidia hasa kaunti saba zilizo karibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako