• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jinsi bahari ya Aktiki ilivyobadilika kuwa ya chumvi

  (GMT+08:00) 2017-06-21 19:15:27

  Katika mamilioni ya miaka iliyopita, bahari ya Aktiki ilikuwa ziwa kubwa lenye maji baridi, haikuwa imeungana na bahari zenye maji ya chumvi. Wanasayansi wa Ujerumani waligundua kuwa baada ya bara lililoko kati ya Greenland na Scottland kuzama mita 50 chini ya usawa wa bahari, maji ya Atlantiki yalianza kuingia kwenye bahari ya Aktiki na kufanya maji ya huko yawe na chumvi.

  Siku hizi kuna eneo kubwa la bahari kati ya Greenland na Scottland, lakini katika mamilioni ya miaka iliyopita, eneo hili lilikuwa nchi kavu. Wakati huo mlango bahari wa Bering pia ulikuwa juu ya usawa wa bahari na kutenga bahari ya Arctic na bahari ya Atlantiki.

  Watafiti wa Taasisi ya Alfred Wegener ya Ujerumani wamesema wamehesabu mchakato wa nchi kavu kuzama mita 200 chini ya maji, na kugundua mchakato huo huenda uliendelea kwa mamilioni ya miaka. Utafiti unaonesha kuwa maji ya chumvi ya bahari ya Atlantiki hayakuingia kwenye bahari ya Aktiki mara moja baada ya nchi kavu kuzama chini ya usawa wa bahari, bali yaliingia baada ya nchi kavu kuzama mita 50 chini ya maji, na tabaka la mchanganyiko wa maji ndio liko kwenye kina hiki.

  Kutokana na tofauti za joto, kiasi cha chumvi na uzito, maji ya baharini yanagawanyika katika matabaka mengi. Kwenye tabaka la mchanganyiko wa maji, joto, kiasi cha chumvi na uzito wa maji huwa ni sawasawa katika sehemu mbalimbali baharini. Ila tu nchi kavu ikizama hadi kufikia tabaka hilo, maji ya chumvi ya bahari ya Atlantiki yataweza kuingia kwenye bahari ya Aktiki.

  Hivi sasa nchi kavu ya kale kati ya Greenland na Scottland imezama mita 500 chini ya maji, isipokuwa Iceland.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako