• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cristiano Ronaldo aibeba Ureno kuongoza kombe la mabara

    (GMT+08:00) 2017-06-22 09:57:57

    Akiwa anasubiria siku yake ya kutoa maelezo kuhusiana na kesi yake inayoendelea ya ukwepaji kulipa kodi jana Cristiano Ronaldo alikuwa na siku njema.

    Ronaldo aliiongoza Ureno kuibamiza Russia bao moja kwa nunge kwenye kombe la mabara. Bao hilo la pekee la Ureno liliwekwa kimiani na mshambuliaji huyo katika kipindi cha kwanza.

    Baada ya mchezo huo kuisha kulipigwa mchezo mwingine kati ya Mexico na Newzealand ambapo hadi mchezo unamalizika Mexico waliibuka kidedea kwa mabao mawili kwa moja.

    Newzealand walitangulia kuuona mlango wa Mexico katika dakika ya 42 kupitia kwa Chris Wood ambapo bao hilo lilidumu kwa kipindi kimoja kwani kipindi cha pili dakika ya 54 Raul Gimenez alisawazisha bao hilo kwa mkwaju mkali sana kabla ya Oribe Pelarta kuifungia Mexico la pili dakika ya 73.

    Kwa matokeo hayo sasa Ureno na Mexico wanalingana alama wote wakiwa na nne huku nafasi ya 3 ikishikiliwa na Urusi wenye alama 3 na Newzealand wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja na sasa wameaga rasmi mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako