• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jaspreet Chatthe kushiriki kuwania pointi za duru ya Pearl of Africa nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2017-06-22 10:00:12

    Bingwa wa Mbio za Magari za Afrika mwaka 2015, Jaspreet Chatthe kutoka Kenya ni miongoni mwa madereva 52 waliojiandikisha kuwania pointi za duru ya Pearl of Africa nchini Uganda mnamo Juni 30 na Julai 1 mwaka 2017.

    Kulingana na orodha ya washiriki ambayo imetolewa na Shirikisho la Mbio za Magari la Uganda (FMU) Chatthe, ambaye anaongoza Mbio za Magari za Afrika za mwaka 2017, ni mmoja wa washiriki 10 wa kigeni waliothibitisha kushiriki.

    Madereva wengine wa kigeni ni bingwa mpya wa Kajiado Rally Manvir Baryan na binamu wa Jaspreet Chatthe, Dilraj Chatthe kutoka Kenya, Fabrice Yoto, Claude Gakwaya na Valery Bukera wa Rwanda, Leroy Gomes na Kleevan Gomes wa Zambia, Giancarlo Davite kutoka Ubelgiji na Roshanali Mohamed wa Burundi. Baadhi ya madereva wakali kutoka Uganda mashindanoni ni Duncan Mubiru na Ronald Ssebugizi.

    Jaspreet anaongoza msimamo wa Mbio za Magari wa Afrika mwaka 2017 kwa pointi 28 baada ya kumaliza Safari Rally nchini Kenya katika nafasi ya pili Machi 17-19 na katika nafasi ya tano kwenye duru ya York Rally nchini Afrika Kusini mnamo Aprili 20-22.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako