• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 100 wauawa katika mapigano mapya Afrika ya kati

    (GMT+08:00) 2017-06-22 10:07:29

    Mapigano mapya yaliyoibuka nchini jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha vifo vya watu karibu 100 na wengine wengi kujeruhiwa.

    Jumanne asubuhi kundi la Anti-Balaka limefanya shambulizi dhidi ya kundi la Seleka kwenye eneo la Baria na kupambana kwa muda wa saa kadhaa, kabla ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa MINUSCA kuingilia kati mapigano hayo.

    Siku moja kabla ya mapigano kutokea, makundi 13 kati ya 14 ya upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yalisaini makubaliano ya kusimamisha vita na serikali ya nchi hiyo mjini Rome, Italia. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, makundi mbalimbali yanatakiwa kusimimisha vita kote nchini chini ya usimamizi wa jumuiya ya kimataifa.

    Habari pia zinasema, uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mashtaka ya uhalifu wa kijinsia dhidi ya walinzi wa amani kutoka Jamhuri ya Congo nchini CAR umegundua "matatizo ya kimfumo", na maofisa wa Congo wataondolewa kutoka kikosi cha MINUSCA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako