• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapokea msaada wa chakula kutoka serikali ya China

    (GMT+08:00) 2017-06-22 16:50:34

    Serikali ya Kenya imepokea tani 7,750 za awamu ya kwanza ya msaada wa chakula kutoka kwa serikali ya China.

    Hafla ya kupokea msaada huo ilifanyika kwenye ghala la nchi kavu la kuhifadhi makontena la Nairobi. Baadhi ya chakula cha msaada kilisafirishwa kwa kutumia reli mpya ya Mombasa-Nairobi ambayo ilijengwa kwa msaada wa China, ikiwa ni mara ya kwanza kwa reli hiyo kusafirisha mizigo.

    Kwa mujibu wa waraka kuhusu serikali ya China kutoa msaada wa chakula wa kibinadamu kwa Kenya uliosainiwa tarehe 27 Machi mjini Nairobi, China itatoa zaidi ya tani elfu 20 za msaada wa chakula kwa Kenya ili kutatua uhaba wa chakula uliotokana na ukame nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako