• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wachangia Euro milioni 2 kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2017-06-22 19:08:29

    Operesheni ya Ulinzi wa Raia na Msaada wa Kibinadamu ya Umoja wa Ulaya (ECHO) imechangia Euro milioni 2 ili kukabiliana na hali ya dharura ya uhaba wa chakula na elimu kwa wakimbizi wa Sudan Kusini wanaoishi nchini Uganda.

    Katika taarifa yake, Idara hiyo imesema kuwa fedha hizo zitatumika kulisaidia Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF kukabiliana na mahitaji makubwa ya lishe bora na elimu kwa watoto wa wakimbizi na wa Uganda.

    Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, zaidi ya wakimbizi laki 7. 5 wa Sudan Kusini wamewasili nchini Uganda kuanzia Julai mwaka jana, huku tayari nchi hiyo ikiwa na zaidi ya wakimbizi laki 9 wa Sudan Kusini tangu mapigano yatokee katika nchi hiyo mwezi Disemba mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako