• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yafanya kampeni kuvutia watalii wa China

    (GMT+08:00) 2017-06-22 20:18:18

    Rwanda imeanza kampeni za kutafuta ongezeko la watalii wa China.

    Rwanda ilijiunga nan chi nyingine 50 kwenye maonyesho ya siku tatu ya kibiashara na huduma mjini Beijing China kupigia debe vivutio vyake vya utalii.

    Akiongea kwenye maonyesho hayo, balozi wa Rwanda nchini China, Virgile Rwanyagatare, alisema ni fursa zuri ya nchi yake kujitangaza na kuvutia watalii.

    Rwanda na Ivory Coast ndio nzhi za pekee za Afrika zilizoshiriki maonyesho hayo.

    Rwanyagatare alisema wageni wanaozuru Rwanda wanavutiwa sio tu na wanyama na misitu lakini pia na chai na kahawa yake.

    Alisema wachina wengi wameahidi kushiriki hafka ya mwaka huu ya 'Kwita Izina' yaani kutoa majina kwa sokwe nchini Rwanda mwezi Septemba.

    Hata hivyo alisema Rwanda bado inahitaji kuwekeza kwenye miundo mbinu kama vile barabara, hoteli na viwanja vya ndege ili kutoa huduma bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako