• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Vijana waliokopeshwa Butaleja Uganda wakosa kulipa

    (GMT+08:00) 2017-06-22 20:18:35

    Maafisa wa serikali katika wilaya ya Butaleja nchini Uganda wanasema wamepata asilimia 23 tu ya malipo ya mikopo kutoka kwa vikundi vya vijana.

    Wilaya hiyo ilipokea shilingi milioni 218 za kutoa mikopo kwa vijana katika mwaka wa fedha 2015-2016.

    Baada ya kupokea fedha hizo maafisa husika walichagua vikundi 40 wenye miradi inayohitumu kupewa mikopo na kuwapa kati ya shilingi milioni 3 na 5.

    Lakini hata hivyo sasa kamishena wa wilaya hiyo Richard Gulume Balyaino, amesema waliofaidika wamekosa kulipa na wengine kwenda mafichoni.

    Gulume amesema serikali sasa haitoi tena fedha za mikopo kwa vijana wilayani humo baada ya kukosa kulipa hali ambayo imepelekea kukosa milioni 450 ambazo ingepata mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako