• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China aeleza msimamo wa China kuhusu suala la Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:25:05

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Wang Yi jana alikutana na mwenzake wa Jordan Bw Ayman Safadi na kumweleza msimamo wa China kuhusu suala la Mashariki ya Kati.

    Bw Wang amesema hali ya kukosekana kwa utulivu Mashariki ya Kati inatishia amani na maendeleo ya dunia, na China inapenda amani na utulivu virejee mapema iwezekanavyo.

    Bw Wang ameongeza kuwa China inauunga mkono kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kikanda katika kupambana na ugaidi. Na inapendekeza kutafuta njia mwafaka ya kuendeleza uchumi, na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa ifuatilie zaidi maeneleo ya Mashriki ya Kati.

    Amesema China ni mwenzi wa kuaminika wa nchi za kiarabu, na inapenda kutoa mchango katika kuondoa ugaidi na kuzisaidia kuleta ustawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako