• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumaini ya Cameroon yafufuka kwa matokeo ya jana ya Confedaration Cup

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:54:15

    Matokeo ya jana katika kundi B la michuano ya Confedaration Cup yamezidi kulifanya kundi hilo kuwa gumu zaidi kwani sasa timu zote nne zina nafasi ya kufuzu kucheza nusu fainali

    Mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya vibonde wa kundi hilo ambao wote walifungwa katika mchezo wao wa kwanza timu ya Cameroon waliokuwa uwanjani kuwakabili Australia.

    Mchezo huo uliisha kwa suluhu ya bao moja kwa moja ambapo bao la Cameroon lilifungwa dakika ya 45 na Andre Anguissa na baadae kipindi cha pili Mark Milligan aliisawazishia Australia.

    Baadae Chile waliikabili Ujerumani ambapo matokeo yalifanana na mchezo wa kwanza baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya bao moja kwa moja.

    Chile walitangulia kupata bao dakika ya 6 kupitia mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez kabla ya Ujerumani kusawazisha dakika ya 41 kupitia kwa Lars Stindi.

    Kwa matokeo hayo Kundi B Ujerumani na Chile wanaongoza wakiwa na alama nne nne lakini Cameroon na Australia wana alama moja moja na kama wakishinda michezo yao ya mwisho watakuwa na alama nne sawa na walioko juu yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako