• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taifa Stars kimekwenda Afrika Kusini kushiriki michuano ya Cosafa

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:58:33

    Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Tanzania 'Taifa Stars', kimeondoka jana kuelekea nchini Afrika Kusini kushiriki michuano Kombe la Cosafa.

    Akiongea na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam jana, kocha wa Mkuu Salum Mayanga amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri kiafya hivyo wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo.

    Taifa Stars wao wamepangwa katika kundi A na wapinzania wao katika kundi hilo ni timu za Mauritius, Malawi na Angola.

    Katika kundi B kuna timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar pamoja na Zimbabwe, michuano hiyo itaanza kutimua vumbu kuanzia Juni 25.

    Mwenyeji Afrika ya kusini, Botswana, Zambia, Namibia, Lesotho na Swaziland watacheza michezo maalumu ya mchujo (play off) kuwania kuingia robo fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako