• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China azungumzia suala la wakimbizi wa Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2017-06-24 17:10:12

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana huko Beirut alipokutana na waandishi wa habari pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Lebanon Bw. Gebran Bassil, ameeleza msimamo wa China kuhusu suala la wakimbizi wa Mashariki ya Kati.

    Bw. Wang Yi amesema nchi nyingi za Mashariki ya Kati ikiwemo Lebanon zimefanya jitihada kubwa kwa ajili ya kuwapokea wakimbizi kutoka Syria na nchi nyingine. Lakini wakimbizi si wahamiaji, ambao wanapenda kurudi kwenye nchi zao na kujenga upya makazi yao. Hayo ni matumaini ya kila mkimbiziambayo yanalingana na mwelekeo wa juhudi za kibinadamu duniani, vilevile ni sehemu moja ya azimio la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu utatuzi wa suala la Syria kwa njia ya kisiasa.

    Bw. Wang amesema China inapenda kuzisaidia nchi zinazowapokea wakimbizi kuongeza uwezo wa kukabiliana na changamato, na kutoa mchango wake kwa ajili ya kuwasadia wakimbizi warudi nyumbani mwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako