• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majeshi ya Iraq yaendelea kusonga mbele kuelekea katikati ya Mosul huku yakikumbana na upinzani mkali

    (GMT+08:00) 2017-06-26 09:27:53

    Majeshi ya Iraq yanayoendelea kupambana na wapiganaji wa kundi la IS jana waliendelea kusonga mbele kuelekea katikati ya mji wa Mosul kwenye eneo lenye wakazi wengi.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa operesheni za pamoja Brigedia Jenerali Yahya Rasoul amesema hadi sasa ni asilimia moja tu ya mji wa Mosul iko mikononi wa wapiganaji wa kundi la IS, na majeshi ya Iraq yanasonga mbele kuelekea sehemu hiyo kutoka pande mbalimbali.

    Vikosi mbalimbali vya serikali ikiwa ni pamoja na vikosi vya jeshi, polisi na vikosi maalum vinapambana katika maeneo tofauti, lakini mapambano makali yanaendeshwa na kikosi cha komando karibu na hospitali kuu ya eneo la al-Shifaa ambako wapiganaji wengi wa kundi la IS wamejificha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako