• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 143 wafariki baada ya lori la mafuta kulipuka Pakistan

    (GMT+08:00) 2017-06-26 10:33:29

    Watu wasiopungua 143 wamefariki dunia na wengine 156 wamejeruhiwa baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka katika wilaya ya Bahawalpur mkoani Punjab, mashariki mwa Pakistan.

    Daktari wa hospitali ya Victoria Javaid Iqbal amesema idadi ya vifo imefikia 143 baada ya majeruhi watatu walioungua vibaya kufariki wakati wa matibabu. Huenda idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na hali mbaya ya majeruhi wengine zaidi ya 20.

    Polisi wamesema janga hilo limetokea jana asubuhi baada ya lori lililobeba lita elfu 50 za mafuta kuacha barabara kuu ya Ahmad Pur Sharqia na kupinduka kutokana na kupasuka kwa gurudumu, umbali wa kilomita 400 kutoka kusini mwa Lahore, kabla ya kuwaka moto na kulipuka wakati watu wengi walikuwa wakikimbilia eneo la ajali na kukusanya mafuta yaliyovuja kutoka lori hilo.

    Uchunguzi wa polisi unaonesha kuwa moto huo ulianza baada ya mtu mmoja kwenye eneo la ajali kuwasha sigara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako