• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNEP yavutiwa na mafanikio ya China ya kudhibiti kuenea kwa jangwa

    (GMT+08:00) 2017-06-27 16:04:53

    Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Erik Solheim amesema mafanikio ya China katika kurejesha misitu katika maeneo ya jangwa ni mfano kwa nchi nyingine katika kukabiliana na athari za kuenea kwa jangwa.

    Bw. Solheim amesema, badala ya kulichukulia suala la kuenea kwa jangwa kama tatizo, inapaswa kutazamwa kama fursa ya maendeleo ya uchumi na kutoa nafasi za ajira.

    Bw. Solheim alikuwa akizungumzia jangwa la Kubuqi ambalo ni la saba kwa ukubwa nchini China lililoko kwenye mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, ambapo katika miongo mitatu iliyopita, robo ya eneo la jangwa hilo imegeuzwa kuwa msitu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako