• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Huduma ya intanenti haitakatizwa wakati wa uchaguzi Kenya

    (GMT+08:00) 2017-06-27 19:09:34

    Biashara na shughuli zinazotegemea mtandao wa intanenti nchini Kenya zitaendelea kama kawaidia wakati wa uchaguzi mkuu mwezi agosti.

    Mamlaka ya Mawasiliano Kenya imehakikishia wadau hao kwamba kuwa intanenti haitapotea katika siku ya uchaguzi mkuu.

    Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo CAK, Prof Francis Wangusi, amesema kuwa huduma za mtandao zitakuwepo kama kawaida Agosti 8 Wakenya watakapopiga kura kuwachagua viongozi wapya nchini.

    Kampuni zote tatu za mawasiliano ya simu nchini – Safaricom, Airtel na Telkom (zamani ikijulikana kama Orange) – zimehusishwa ili kuhakikisha kuwepo kwa mtandao kwa minajili ya kusambaza matokeo ya kura kwa njia ya kielektroniki.

    Aidha, Prof Wangusi alisema simu zitakazotumiwa kutuma matokeo zitastahili kusajiliwa ili kuonyesha kituo cha kupiga kura ambako matokeo yatatoka, na hivyo kuimarisha uadilifu.

    Kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Prof Abdi Guliye, alisema kuwa vifaa 45,000 vya kutambua wapiga kura (BVR) vitatumika Agosti 8.

    Tayari 11,000 vilitumika katika zoezi la kuthibitisha maelezo ya wapiga kura lililokamilika Ijumaa iliyopita.

    Vifaa vingine zaidi vya habari na mawasiliano (ICTs) vinaendelea kuwasili nchini; vya hivi punde vikiwa ni seva mbili za kuhifadhi data zilizowasili wiki hii, moja itakayotumika kama hifadhi kuu na nyingine hifadhi mbadala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako