• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yashambulia miundombinu ya kundi la Hamas huko Gaza

    (GMT+08:00) 2017-06-27 19:12:20

    Israel imefanya shambulizi dhidi ya miundombinu ya kijeshi ya kundi la Hamas usiku wa kuamkia leo.

    Jeshi la nchi hiyo limesema, hatua hiyo imechukuliwa kujibu shambulizi la kombora lililoanguka katika eneo la Sha'ar HaNegev, kusini mwa Israel bila ya kusababisha majeruhi au hasara yoyote.

    Msemaji wa kikosi hicho amesema, ndege za kivita za jeshi la anga la Israel zililenga miundombinu miwili ya kijeshi inayomilikiwa na kundi la Hamas katika eneo la kaskazini na kusini mwa Ukanda wa Gaza.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya huko, hakuna ripoti yoyote ya majeruhi wala vifo vilivyotokana na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako