• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wanane wauawa katika mlipuko uliotokea barabarani katika mji wa Lamu Kenya

    (GMT+08:00) 2017-06-28 09:57:12

    Maofisa wa usalama wa Kenya wameanza msako dhidi ya washukiwa wa Kundi la Al-Shabaab wanaotuhumiwa kujihusisha na mauaji ya polisi wanne na watoto wanne wanafunzi katika kaunti ya Lamu.

    Kamanda wa polisi Bw Phillip Tuimur amesema wahanga hao walifariki papo hapo baada ya lori waliokuwa wakisafiria kukanyaga bomu la ardhini katika barabara ya Marrani-Kiunga. Hivi sasa maofisa wa polisi wametumwa kufanya uchunguzi na kuwahamisha majeruhi.

    Ripoti imesema maofisa 17 wa polisi walijeruhiwa katika tukio hiyo na wameondolewa kutoka kwenye eneo la tukio. Tukio hilo limetokea wakati watoto wakirudi shuleni baada ya mapumziko.

    Kikosi cha ulinzi cha Kenya, timu maalumu ya maofisa wa polisi pamoja na kikosi maalum cha doria mpakani cha Mangai wameimarisha hatua za usalama, hali iliyofanya kundi la Al Shabaab kubadilisha mbinu zake na kutumia mabomu ya kutegwa ardhini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako