• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mageuzi ya China yahitaji ushiriki wa mtaji wa nchi za nje

    (GMT+08:00) 2017-06-28 17:48:11

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang amesema mageuzi ya China yanahitaji ushiriki wa mtaji, kampuni, na busara za nchi za kigeni, na kuahisi urahisi wa kuingia kwenye soko la China na uwiano katika biashara.

    Li Keqiang amesema hayo kwenye mkutano wa wakuu wa biashara unaoendelea kando ya Mkutano wa Mwaka wa Davos wa majira ya joto unaofanyika Dalian hapa China. Li amesema, siku zote mageuzi ya China yanakwenda sambamba na kufungua zaidi mlango, hivyo China inazikaribisha kampuni za kigeni kushiriki katika mageuzi, na kwamba China itapunguza zaidi vizuizi vya huduma ili kuchochea injini mpya za ukuaji.

    Akizungumzia kuhusu mtandao wa internet plus, Li Keqiang amesema China inayakaribisha makampuni ya kigeni kushiriki kwenye mpango huo. Amesema wawekezaji wa kigeni wana nafasi kubwa kwa maendeleo katika mtandao wa Internet Plus, ikiwemo mawasiliano ya simu na biashara ya kuvuka mpaka ya bidhaa za kielektroniki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako