• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la kwanza la WHO kuhusu afya barani Afrika lamalizika

    (GMT+08:00) 2017-06-29 10:12:46

    Kongamano la kwanza la Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu afya barani Afrika limemalizika jana mjini Kigali, Rwanda, kwa kutoa ahadi ya kutimiza upatikanaji wa huduma za afya kwa wote barani humo.

    Kongamano hilo la siku mbili lilikutanisha wajumbe zaidi ya 700 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wasomi, mawaziri wa afya, mashirika ya kiserikali na ya kijamii, na sekta binafsi. Wajumbe hao walijadili masuala muhimu ikiwemo kutumia kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa wote kama njia kuu ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu kuhusu afya, ambayo yanahakikisha maisha bora na kuinua afya ya watu wote katika umri wote, na kuimarisha na kudumisha maendeleo ya nguvukazi kwenye sekta ya afya.

    Wajumbe hao pia wametoa wito kwa serikali barani Afrika kuongoza na kusimamia vitendo vinavyolenga kujenga majukwaa ya uratibu na mfumo wa kanuni ili kutimiza upatikanaji wa huduma za afya, kuongeza uwekezaji wa ndani, na kusimamia na kutoa ripoti za maendeleo yanayopatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako