• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la China Southern laanzisha ukaguzi wa abiria kutumia mashine za kutambua sura

    (GMT+08:00) 2017-06-29 18:13:11

    Shirika la ndege la China Southern limekuwa ni shirika la kwanza kutumia teknolojia ya kutambua abiria kwa kutumia mashine, teknolojia iliyoanza kutumika jana kwenye uwanja wa ndege wa Nanyang, Mkoani Henan.

    Mjumbe wa shirika la kimataifa la usafiri wa ndege IATA Bw Hou Kan, amesema tiketi za kielektroniki, risiti za kielektroniki na utambuzi wa sura za abiria kwa kutumia kamera, utarahisisha sana utaratibu wa kuruhusu abiria kuingia kwenye ndege.

    Meneja wa Shirika la ndege la China Southern Bw Huang Wenqing amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuzuia wizi wa taarifa binafsi za abiria.

    Utaratibu huo unatarajiwa kuanza kutumika baadaye kwenye uwanja mpya wa ndege wa Beijing na viwanja vingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako