• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ugonjwa wa kipindupindu wasababisha vifo vya watu elfu 1.4 nchini Yemen

    (GMT+08:00) 2017-06-29 19:34:05

    Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa katika miezi miwili iliyopita, watu karibu elfu 1.4 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, na idadi ya watu wanaodhaniwa kuambukizwa ugonjwa huo imeongezeka hadi kufikia laki 2.18.

    Kabla ya hapo, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bibi Margaret Chan na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa Bw. Antony Lake walitoa taarifa ya pamoja ikisema, idadi ya watu wanaodhaniw kuambukizwa kipindupindu inaongezeka kwa watu elfu 5 kila siku nchini Yemen, na kufanya nchi hiyo ikabiliwe na maambukizi makubwa zaidi duniani.

    Takwimu za WHO zinaonesha kuwa mlipuko wa kipindupindu ulianza mwishoni mwa mwezi wa Aprili mwaka huu katika mji wa Sanaa, na kwenye mikoa ya kaskazini inayodhibitiwa na kundi la Hussein. Hivi sasa watu zaidi ya milioni 7.6 wanaishi katika sehemu zinazoathiriwa na maambukizi, wakiwemo wakimbizi milioni 3 wanaoweza kuambukizwa ugonjwa huo kwa urahisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako