• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wahimiza kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya elimu

    (GMT+08:00) 2017-06-29 19:34:43

    Mwenyekiti wa mkutano wa 71 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Peter Thomsen na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja huo Bibi Irina Bokova, wamehimiza kutimiza malengo husika ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 kupitia kuongeza mitaji, kuhimiza usawa wa kijinsia na kusukuma mbele ubunifu wa elimu.

    Bw. Thomsen amesema hayo katika shughuli ya kuhimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, huku akisema elimu ni nguvu kuu ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu.

    Bibi Bokova amesema elimu ni haki ya msingi ya binadamu, pia ni msingi wa maendeleo endelevu unaohuisha amani na matumaini, hivyo ni kiini cha ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. Ameongeza kuwa wanawake wanakabiliwa na vikwazo vingi katika elimu, huku akizitaka serikali za nchi mbalimbali kutoa kipaumbele katika elimu na kuzingatia usawa wa kijinsia na kuhimiza elimu ya maisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako