• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bayern waamua kumsamehe Alexis Sanchez

    (GMT+08:00) 2017-06-30 08:58:53

    Vita vya usajili bado vinaendelea na kila kukicha kumekuwa na habari mpya huku kila timu ikijaribu kumnunua mchezaji mpya ili kuimarisha vikosi vyao.

    Suala la Alexis Sanchez bado linapasua kichwa watu wengi kwani hawajui kama atabaki Arsenal, ataenda Chelsea, Man City au atahamia Bayern Munich.

    Lakini sasa Bayern Munich ambao kwa siku za karibuni wamekuwa wakihusishwa sana na Sanchez wameamua kutoa duku duku lao la moyoni kuhusu masuala ya usajili.

    Bayern wanasema wao sera zao kwa wakati wote ni kununua wachezaji makinda kati ya umri wa miaka 20 hadi 22 na hiyo ndio namna wanavyoijenga klabu yao.

    Lakini wakasema hawako tayari kutumia pesa nyingi sana kwa ajili ya kununua aina ya wachezaji ambao umri wao umeenda sana na kufikisha miaka 29 hadi 30.

    Japokuwa Raisi wa klabu hiyo Uli Hoeness hakumtaja mtu moja kwa moja wakati anayasema hayo, lakini inafahamika Bayern walitajwa kumtaka Sanchez ambaye ana miaka 29 na bei yake ni kubwa sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako