• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Ulaya wakutana Berlin kutafuta umoja kabla ya mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:20:47

    Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekutana jana mjini Berlin kutafuta sauti moja kabla ya mkutano wa kundi la nchi 20 utakaofanyika Julai 7 na 8 mjini Hamburg Ujerumani.

    Baada ya mkutano ulioitishwa na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel, viongozi wa Ufaransa, Uingereza, Italia, Hispania, Uholanzi, Norway na Umoja wa Ulaya wamesema watashirikiana kwenye suala la mabadiliko ya hali ya hewa na biashara huria.

    Mapema jana Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel aliliambia bunge la Ujerumani kuwa kwenye mkutano huo, ataweka mkazo kwenye biashara huria, ushirikiano wa kimataifa na makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako