• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya bidhaa za China kusukuma mbele biashara kati ya China na Kenya

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:53:58

    Awamu ya tatu ya Wiki ya biashara ya China nchini Kenya ilifunguliwa jana mjini Nairobi kwa lengo la kusukuma mbele biashara kati ya China na Kenya.

    Wafanyabiashara zaidi ya 400 wa China kutoka sekta mbalimbali zikiwemo uzalishaji, vifaa vya ujenzi, kauri, vipuri vya magari na bidhaa za walaji, wanaonesha bidhaa kwenye maonesho hayo ya siku tatu.

    Mkurugenzi wa kampuni ya MIE Events inayoandaa maonesho hayo Bw. David Wang, amesema China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Kenya, na kuwamba maonesho ya bidhaa za China yatasaidia kusukuma mbele biashara kati ya pande mbili kwa kuwawezesha wafanyabiashara wa Kenya kuwasiliana na wenzao kutoka China bila kusafiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako