• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akagua gwaride la askari wa ulinzi wa jeshi la ukombozi la China mkoani Hong Kong

    (GMT+08:00) 2017-06-30 16:26:31

    Rais Xi Jinping wa China leo amekagua kikosi cha askari wa Jeshi la Ukombozi la China katika mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong, ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 20 tangu Hong Kong irejeshwe China.

    Zaidi ya askari na maofisa 3,100 walishiriki kwenye gwaride hilo, na zaidi ya silaha 100 za kijeshi zilionyeshwa.

    Rais Xi ambaye pia ni Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, amekagua gwaride hilo akiongozana na Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Hong Kong, Tan Benhong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako