• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 15 wa kundi la Taliban wauawa katika shambulizi lililofanywa na jeshi la anga la Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-06-30 18:19:40

    Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema, wapiganaji zaidi ya 15 wa kundi la Taliban wameuawa baada ya jeshi la anga la nchi hiyo kushambulia maficho yao mkoani Uruzgan.

    Helikopta za jeshi la nchi hiyo zilishambulia kituo cha wapiganaji kilichoko sehemu ya Mir Abad huko Tirin Kot, mji mkuu wa Uruzgan na kusababisha vifo vya wapiganaji 15.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo, askari wa jeshi hilo pia wamegundua na kuondoa bomu lililotegwa kwenye eneo la Kotwali mjini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako