• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa bunge la Afrika Kusini apanga upya ratiba ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais Jocob Zuma

    (GMT+08:00) 2017-07-03 08:39:30

    Spika wa bunge la Afrika kusini bibi Baleka Mbete amepanga Agosti 8 kuwa tarehe mpya ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais Jocob Zuma wa nchi hiyo, badala ya Agosti 3 iliyotangazwa awali. Uamuzi huo ulitolewa kufuatia majadiliano na vyama vya kisiasa bungeni. Juni 22 mahakama ya kikatiba ya nchi hiyo ilimpa mamlaka Bibi Mbete kuamua kama kura hiyo itafanyika kwa njia ya siri au la, na Ijumaa iliyopita Bibi Mbete alisema kuwa bunge linajadili ombi lililotolewa na upinzani la kutaka kura hiyo ifanyike kwa njia ya siri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako