• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa kuunga mkono kikosi cha kupambana na ugaidi cha kundi la nchi tano la Sahel

    (GMT+08:00) 2017-07-03 09:24:57

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema nchi yake itaunga mkono kikosi cha kupambana na ugaidi cha kundi la nchi tano la Sahel.

    Akizungumza katika mkutano maalum wa viongozi wa kundi hilo uliofanyika jana kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako, Rais Macron amesema kuwa Ufaransa itatoa vifaa vyenye thamani ya Euro milioni 8 ikiwemo maderaya 70 ya kivita, vifaa vya mawasiliano na vya ulinzi wa askari, kabla ya mwisho wa mwaka huu kusaidia mapambano hayo.

    Pia rais Macron amesisitiza kuwa, Ufaransa itaendelea kuisaidia Mali na eneo la Sahel kutafuta amani na utulivu na kutimiza maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako